Tuesday, 23 September 2014

PIGO ARSENAL, DEBUCHY KUWA NJE KATI YA WIKI SITA HADI MIEZI MITATU


BEKI wa pembeni wa Arsenal, Mfaransa Mathieu Debuchy  anaweza kuwa nje ya Uwanja hadi Krisimasi baada ya kuumia enka dhidi ya Manchester City mwishoni mwa wiki iliyopita.
Kocha Arsene Wenger amesema kwamba Debuchy alitarajiwa kwenda kufanyiwa uchunguzi kama atahitaji upausaji wa kifundo chake cha mguu jana jioni ambao utatoa majibu atakaa nje kwa muda gani.
Ikiwa hatahitaji upasuaji, itamchukua wiki sita nje ya Uwanja kabla ya kurejea dimbani, lakini kama atapigwa 'kisu' atakuwa nje kwa angalau miezi mitatu.
Mathieu Debuchy akiugulia maumivu baada ya kuumia wiki iliyopita dhidi ya Manchester City

LIVERPOOL YACHARANGWA 3-1 NA WEST HAM

LIVERPOOL YACHARANGWA 3-1 NA WEST HAM

LIVERPOOL imefumuliwa mabao 3-1 na West Ham United katika Ligi Kuu ya England usiku wa leo Uwanja wa Upton Park.
Hammers walipata bao la kwanza kupitia kwa Winston Reid dakika ya pili, kabla ya Diafra Sakho kufunga la pili dakika ya tano.
Raheem Sterling aliwafungia Wekundu wa Anfield waliotinga jezi za njano leo dakika ya 26 kabla ya mchezaji mpya, Morgan Amalfitano kufunga bao la tatu.
Kikosi cha West Ham kilikuwa: Adrian, Demel/Jenkinson dk61, Reid, Tomkins, Cresswell, Noble, Kouyate, Song, Downing, Sakho na Valencia. 
Liverpool: Mignolet, Manquillo/Sakho dk22, Skrtel, Lovren, Moreno, Gerrard, Henderson, Lucas/Lallana dk45, Sterling, Borinin na Balotelli.
Mario Balotelli akiruka kuupisha mpira uliopigwa na Raheem Sterling upite katika mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya West Ham. Liverpool ililala 3-1.

FALCAO AKIUMIA TU, MKATABA WAKE UNAVUNJWA MAN UNITED

FALCAO AKIUMIA TU, MKATABA WAKE UNAVUNJWA MAN UNITED

KLABU ya Manchester United inaweza kumrudisha Radamel Falcao katika klabu yake, Monaco iwapo ataumia goti lililomfanya awe nje ya Uwanja kwa muda mrefu msimu uliopita.
Mshambuliaji huyo Colombia amehamia Old Trafford kwa mkopo wa Pauni Milioni 6 mwaka mmoja akikamilisha uhamisho wake siku ya mwisho na analipwa wastani wa Pauni 300,000 kwa wiki. 
Lakini United katika kuhakikisha uwezekezaji huo hauwi wa hasara, katika Mkataba wao wakaweka kipengele cha kumrudisha iwapo ataumia tena.

Radamel Falcao alicheza kwa dakika 20 dhidi ya QPR, akitokea benchi katika mechi yake yake ya kwanza Manchester United

COASTAL UNION YAREJESHA FURAHA JANGWANI, WAING’ANG’ANIA SIMBA SC 2-2 TAIFA

COASTAL UNION YAREJESHA FURAHA JANGWANI, WAING’ANG’ANIA SIMBA SC 2-2 TAIFA


MAKOSA ya safu ya ulinzi ya Simba SC, leo yameigharimu timu hiyo kuanza na sare katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na Coastal Union ya Tanga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
Matokeo hayo wazi yatapokewa kwa furaha na wapinzani wa jadi wa Simba SC, Yanga SC ambao jana walianza ligi kwa kichapo cha mabao 2-0 kutoka Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Simba SC ilikwenda kupumzika ikiwa inaongoza mabao mawili, yaliyotiwa kimiani na kiungo Shaaban Kisiga ‘Malone’ na mshambuliaji, Amisi Tambwe, lakini baada ya dakika 90 matokeo yakawa 2-2.
Karate, au soka? Kiungo wa Simba SC, Ramadhani SIngano 'Messi' katikati ya wachezaji wa Coastal, Sabri Rashid kulia na Ayoub Yahya katika mchezo wa leo

Mabao yote ya Simba SC inayofundishwa na Mzambia, Patrick Phiri akisaidiwa na wazalendo Suleiman Matola na Iddi Pazi ‘Father’ yalitokana na jitihada za mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC, Emmanuel Okwi.
Kisiga alifunga bao zuri la kwanza akimtungua Shaaban mwenzake, mtoto wa mzee Hassan Kado kwa mpira wa adhabu dakika ya sita, baada ya Okwi kuangushwa nje kidogo ya boksi.
Mfungaji bora wa msimu uliopita, Mrundi Tambwe akaanza msimu na bao kuashiria hataki kuvua ‘kiatu cha dhahabu’ baada ya kuunganisha vizuri kwa kichwa krosi ya Mganda, Okwi dakika ya 36.
Coastal Union nao walipoteza nafasi mbili nzuri za kufunga kipindi cha kwanza, kwanza dakika ya tatu baada ya Mkenya, Itubu Imbem kuunganishia juu ya lango krosi ya Hamad Juma na baadaye Joseph Mahundi akashindwa kuunganisha krosi ya Mkenya huyo dakika ya 29.
Bao la kwanza; Shaaban Kisiga akishangilia na Ramadhani Singano 'Messi' kushoto baada ya kufunga bao la kuongoza
Amisi Tambwe akimtoka beki wa Coastal, Mbwana Hamisi 'Kibacha'
Tambwe akishangilia baada ya kufunga bao la pili
Emmanuel Okwi akimkimbiza beki wa Coastal, Sabri Rashid

Lakini kipindi cha pili, mambo yalibadilika na Wagosi wa Kaya wakauteka mchezo. Mshambuliaji wa Uganda, Lutimba Yayo Kato aliifungia bao la kwanza Coastal dakika ya 69, akitumia udhaifu wa mabeki wa Simba SC kujisahau baada ya kiungo wao, Pierre Kwizera kuchezewa faulo.
Mabeki wa Simba SC walitulia kumsikilizia refa Jacob Adongo wa Mara apige filimbi baada ya Kwizera kuchezewa rafu, lakini ‘akakausha’ na Yayo akafunga.
Bao hilo, ‘liliitia ndimu’ Coastal inayofundishwa na Wakenya watatu, Yussuf Chipo, akisaidiwa na Ben Mwalala na Razack Ssiwa na kuanza kushambulia kwa kasi, ingawa Simba SC nayo iliendelea kupeleka mashambulizi langoni mwa Wagosi wa Kaya.
Uhuru Suleiman alikosa bao la wazi dakika ya 78 baada ya kutanguliziwa pasi nzuri na Okwi, lakini akiwa amebaki na kipa Kado, akapiga juu.
Mkenya Rama Salim aliisawazishia Coastal dakika ya 83 kwa mpira wa adhabu- baada ya beki Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ kuunawa mpira nje kidogo ya boksi.
Mshambuliaji Paul Kiongera aliyetokea benchi kipindi cha pili alirudi nje anachechemea dakika ya 88 baada ya kuumia kufuatia kugongana na kipa Kado hivyo kumpisha Amri Kiemba.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Ivo Mapunda, Miraj Adam, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka, Joseph Owino, Pierre Kwizera, Haroun Chanongo/Uhuru Suleiman dk58, Shaaban Kisiga ‘Malone’, Amisi Tambwe/Paul Kiongera dk67/Amri Kiemba dk88, Emmanuel Okwi na Ramadhani Singano ‘Messi’.
Coastal Union; Shaaban Kado, Hamad Juma, Sabri Rashid, Abdallah Mfuko, Hamisi Kibacha, Juma Lui, Suleiman Rajab/Yayo Lutimba dk49, Razack Khalfan/Ayoub Athumani dk49, Itubu Imbem, Rama Salim na Joseph Mahundi/Abbas Athumani dk69.

LAMPARD AIPOKONYA TONGE MDOMONI CHELSEA, AIFUNGA MAN CITY KUPATA SARE BILA KUSHANGILIA

LAMPARD AIPOKONYA TONGE MDOMONI CHELSEA, AIFUNGA MAN CITY KUPATA SARE BILA KUSHANGILIA

BAO la dakika za lala salaam la Frank Lampard lineipa sare ya 1-1 Manchester City pungufu dhidi ya timu yake ya zamani, Chelsea jioni hii Uwanja wa Etihad.
Lampard, aliyejiunga na City kwa mkopo kutoka New York City FC baada ya kutemwa na Chelsea mwishoni mwa msimu, hakushangilia baada ya kufunga bao hilo dakika ya 85.
Andre Schurrle alitangulia kuifungia Chelsea dakika ya 71, muda mfupi baada ya Pablo Zabaleta kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano kwa kucheza rafu. 
Frank Lampard hakutaka kushangilia baada ya kufungia Manchester City dhidi ya klabu yake ya zamani aliyoichezea kwa miaka 13 

Man City: Hart, Zabaleta, Kompany, Mangala, Kolarov/Lampard dk78, Milner, Fernandinho/Jesus Navas dk73, Toure, Silva, Dzeko/Sagna dk70, Aguero. 
Chelsea: Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Fabregas, Matic, Ramires/Schurrle dk63, Willian/Mikel dk63, Hazard na Costa/Drogba dk86.