BEKI
wa pembeni wa Arsenal, Mfaransa Mathieu Debuchy anaweza kuwa nje ya
Uwanja hadi Krisimasi baada ya kuumia enka dhidi ya Manchester City
mwishoni mwa wiki iliyopita.
Kocha
Arsene Wenger amesema kwamba Debuchy alitarajiwa kwenda kufanyiwa
uchunguzi kama atahitaji upausaji wa kifundo chake cha mguu jana jioni
ambao utatoa majibu atakaa nje kwa muda gani.
Ikiwa
hatahitaji upasuaji, itamchukua wiki sita nje ya Uwanja kabla ya
kurejea dimbani, lakini kama atapigwa 'kisu' atakuwa nje kwa angalau
miezi mitatu.
No comments:
Post a Comment